Kasipul yaomboleza huku viongozi wakimimina sifa kwa marehemu Charles Were
Friday, 9 May, 2025
Shule ya Msingi ya Karabok, Kaunti ya Homa BayIjumaa, Mei 9, 2025
Wingu la simanzi limetanda kijiji cha Karabok, Oyugis katika eneo Bunge la Kasipul, Kaunti ya Homa Bay.
Wabunge wakiongozwa na Spika wa Bunge la Taifa, Mheshimiwa Dkt. Moses Masika Wetang’ula, wamewasili katika Shule ya Msingi ya Karabok kuhudhuria ibada ya mazishi ya marehemu Mbunge wa Kasipul, Mheshimiwa Sir Charles Ong’ondo Were.
Sherehe hiyo ya heshima ya mwisho inaendelea katika uwanja wa shule hiyo, ikiwa imewakusanya viongozi wa kitaifa, wageni mashuhuri, familia, marafiki na wakaazi wa eneo hilo waliokuja kutoa heshima zao za mwisho kwa mwendazake.
Waheshimiwa, mmoja baada ya mwingine, wamekuwa wakimiminia sifa mwendazake kwa uongozi wake wa mfano, utendakazi wake wa uaminifu, na mchango wake mkubwa katika ustawi wa jamii ya Kasipul.