Mswada wa Watoa Huduma za Rasilmali Pepe wa 2025 (Virtual Assets Service Providers Bill, 2025)

Tuesday, 3 June, 2025

Mswada wa Watoa Huduma za Rasilmali Pepe wa 2025 (Virtual Assets Service Providers Bill, 2025)

𝐔𝐭𝐚𝐧𝐠𝐮𝐥𝐢𝐳𝐢

Mswada wa Watoa Huduma za Rasilmali Pepe Mali (Mswada wa Bunge la Taifa Nambari 15 wa 2025) ni Mswada unaodhaminiwa na Kiongozi wa walio Wengi Bungeni. 

Mswada ulichapishwa tarehe 17 Machi 2025. Ulisomwa kwa mara ya kwanza tarehe 8 Aprili 2025. 

Baada ya hapo, Kamati ya Fedha na Mipango ya Taifa ilikabidhiwa Mswada.

𝐔𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐔𝐦𝐦𝐚

Kamati inatakiwa kuuzingatia Mswada, kualika maoni kutoka kwa umma, na kuandaa ripoti yake na mapendekezo ya marekebisho yoyote inayoona yanafaa.

Katiba inatambua umuhimu wa kushirikisha umma katika kutoa maoni kuhusu masuala ambayo yanawaathiri. Hivyo, *Ibara ya 118(1) (b) ya Katiba ya Kenya* inaelekeza kwamba Bunge lazima iwezeshe ushirikishwaji wa umma na umma lazima ipewe fursa ya kutoa maoni kwenye Mswada kama huu.

Ushirikishwaji wa umma (public participation) ni agizo la kikatiba. Wananchi wako huru kutoa maoni yao kuhusu Mswada huu na wanaweza kuunga mkono Mswada au kupinga Mswada. La muhimu ni kutoa sababu ili Kamati ya Kiidara ya Fedha na Mipango ya Taifa ishughulikie kwa kina maoni yako.

Shughuli hii ya vikao vya umma vitaanza leo 𝐉𝐮𝐦𝐚𝐧𝐧𝐞 𝐭𝐚𝐫𝐞𝐡𝐞 𝟑 𝐉𝐮𝐧𝐢 𝐡𝐚𝐝𝐢 𝐈𝐣𝐮𝐦𝐚𝐚 𝐭𝐚𝐫𝐞𝐡𝐞 𝟔 𝐉𝐮𝐧𝐢, 𝟐𝟎𝟐𝟓 katika Kaunti zifuatazo: 𝐌𝐢𝐠𝐨𝐫𝐢, 𝐁𝐮𝐬𝐢𝐚, 𝐍𝐚𝐧𝐝𝐢, 𝐓𝐫𝐚𝐧𝐬 𝐍𝐳𝐨𝐢𝐚, 𝐌𝐚𝐜𝐡𝐚𝐤𝐨𝐬, 𝐊𝐢𝐚𝐦𝐛𝐮, 𝐌𝐨𝐦𝐛𝐚𝐬𝐚, 𝐊𝐰𝐚𝐥𝐞 𝐧𝐚 𝐊𝐢𝐥𝐢𝐟𝐢.

𝐊𝐮𝐡𝐮𝐬𝐮 𝐌𝐬𝐰𝐚𝐝𝐚

Lengo kuu la Mswada ni kutoa mfumo wa kisheria wa kusimamia watoa huduma za rasilmali pepe.

Mswada unaangazia hatari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi mabaya ya bidhaa na huduma za rasilmali pepe.

Hivyo basi, Mswada unaainisha *Mamlaka ya Masoko ya Mitaji (Capital Markets Authority)* na *Benki Kuu ya Kenya (Central Bank of Kenya)* kama mamlaka kuu za udhibiti wa huduma za rasilmali pepe na watoa huduma za rasilmali pepe.

Kazi za jumla za mamlaka za udhibiti zilizoteuliwa zimetolewa chini ya kifungu cha 7 cha Mswada kujumuisha:

• kutoa leseni kwa watoa huduma za rasilmali pepe

• kusimamia, kusimamia na kufuatilia watoa huduma za rasilmali pepe

• kutoa maelekezo, maagizo na kuchukua hatua za utekelezaji, kama inavyoonekana ni muhimu

• kutoa na kuchapisha matangazo, miongozo, vidokezo vya mwongozo na vyombo vingine

Kwa mujibu wa Mswada, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya biashara ya huduma za rasilmali pepe bila kupata leseni kutoka kwa mamlaka husika.

Mswada unaelekeza kwamba mtu yeyote anayetafuta kufanya biashara ya mtoa huduma za rasilmali pepe atawasilisha maombi ya leseni kwa mamlaka husika ya udhibiti kwa kufuata mahitaji kama inavyoweza kuwekwa na kuambatana na ada iliyowekwa ya maombi. 

𝐇𝐢𝐭𝐢𝐦𝐢𝐬𝐡𝐨

Vikao hivi vya umma vinatoa fursa nzuri kwa wananchi na wadau wote kutoa maoni yao kwenye Mswada huu. Mswada huu bado haujakuwa sheria. Baada ya maoni yote kukusanywa, Kamati itaketi kisha izangatie maoni yenu na kutoa ripoti ambayo itawasilishwa katika Bunge la Taifa. Baadaye, mswada huu utafanyiwa marekebisho kabla kupitishwa kuwa sheria.


Mswada wa Watoa Huduma za Rasilmali Pepe wa 2025 (Virtual Assets Service Providers Bill, 2025)

MORE UPDATES

  • Parliament Begins Funeral Arrangements for Late Ol Kalou MP Hon. David Kiaraho
    Parliament Begins Funeral Arrangements for Late Ol Kalou MP Hon. David
  • Committee to Probe Seven Entities As It Probes Alleged Loss Of Sh9billina From E-Citizen
    Committee to Probe Seven Entities As It Probes Alleged Loss Of Sh9billina
  • House committee steps up peace drive in Isiolo County.
    House committee steps up peace drive in Isiolo County.
  • Nationwide Public Participation Exercise On The Public Participation Bill
    Nationwide Public Participation Exercise On The Public Participation Bill
  • No Charlatans Will Be Allowed To Operate In Kenya, Public Work Ps Assures Housing Committee
    No Charlatans Will Be Allowed To Operate In Kenya, Public Work Ps Assures
  • Address Bomayangu Platform Bottlenecks, Housing Committee Tells State Department
    Address Bomayangu Platform Bottlenecks, Housing Committee Tells State